Huwezi kufanya biashara bila kulipa au kulipwa. Kama mfanyabiashara wa kimataifa, unahitaji kujua, na kuwa na njia mbalimbali za kufanya au kupokea malipo ili kuweza kufanya biashara na kampuni mbalimbali. Katika makala hii, tunakuletea analysis ya njia mbali mbali zinazotumika kimataifa ili kufanikisha biashara yako. Vile vile tunakupatia faida na changamoto (pros and cons) za kila njia, ili kukuwezesha kuelewa kwa usahihi kabla ya kutumia njia yoyote.
Je ni kwa nini mfanyabiashara unahitaji njia tofauti za malipo?
Kuna maelfu ya sharia za kimataifa zinazosimamia biashara na malipo. Hata hivyo, njia bora ya malipo inategemea na muuzaji/mnunuaji alipo, na matarajio yake. Vile vile wauzaji mara zote huwa wanatafuta njia bora na rahisi katika kuuza na kupokea fedha. Hivyo hii husababisha tofauti kati ya muuzaji mmoja na mwingine, inaweza kuwa ndani ya nchi moja au nchi/bara tofauti. Kuwa na uwezo wa njia mbadala za kutoa na kupokea malipo inakuwezesha kufanya malipo kwa muda na wakati mwingine kwa fedha ya nchi husika hivyo kupelekea wauzaji kufurahia kufanya biashara na wewe. Hii ni njia rahisi ya kutengeneza uaminifu katika biashara na kukuweka wewe na biashara yako katika nafasi nzuri kiushindani. Hebu tuone njia hizi kwa undani
Wire Transfer
Wire transfer ni utaratibu wa malipo kati ya benki na benki ambao unatumika kutuma pesa kutoka akaunti moja kwenda nyingine. Huu ni utaratibu rahisi wa kutuma pesa kimataifa kwani haihitaji mtu kati ili kushughulikia muamala. Kwa utaratibu huu, mpokeaji anaweza kupokea pesa ndani ya siku 1 mpaka 2.
- Faida zake: Utaratibu huu unapendwa na wafanyabiashara kwa sababu ya urahisi na uharaka. Vile vile taratibu katika nchi zote duniani zinahitaji taarifa za uhakiki za mtumaji na mpokeaji hivyo kufanya kuwa salama zaidi.
- Changamoto: Gharama ya wire transfer ni kubwa sana kulinganisha na njia nyingine. Mara nyingi huwa kuna gharama kwa mtumaji na mpokeaji na wakati mwingine inaweza kuwepo gharama ya benki ya kati kama imehusishwa.
Credit and Debit Card
Debit na Credit cards hutumia mtoa huduma wa kati ili kufanikisha malipo. Watoa huduma hawa (payment processors) mara nyingi ni Visa na Mastercard. Mlipaji anaweza kutumia kadi yake kulipia huduma kwenye “point of service (POS)” au kwa kuingiza namba za kadi kwenye tovuti ya muuzaji. Benki inayotoa huduma hukata makato ya muamala kila huduma inapotolewa
- Faida: Malipo hufanyika kwa haraka sana. Njia hii haina haja ya mtumaji kwenda benki kwani anaweza akafanya malipo mwenyewe kwenye kompyuta au simu yake
- Changamoto: Mara nyingi benki huweka kiwango cha mwisho “limit” cha kutoa pesa kwenye kadi hivyo inaweza ikawa chanagamto kulipia malipo makubwa
Digital Wallet
Digital Wallet ni mifumo inayokuwezesha kuweka pesa na kufanya malipo kwa haraka kwa kutumia simu. Mfano wa hizi digital wallet ni Apple Pay, Paypal, Google Pay, Venmo, MPesa, Tigo Pesa nakadhalika. Mifumo hii inawezesha kufanya malipo kwa haraka ulimwenguni kote bila kuhusisha akaunti ya benki.
- Faida: Digital wallet zina usalama mkubwa sana kwani mtumiaji anaamua kuweka kiasi cha pesa tu anachohitaji kutumia.
- Changamoto: Baadhi ya mifumo hii inafanya kazi kwenye nchi chache, hivyo kufanya mtumiaji kushindwa kuitumia akiwa kwenye nchi ambayo hazitumiki. Vile vile mifumo hii inakata makato kwa huduma inayotolewa
Cryptocurrency
Cryptocurreny ni mfumo mpya wa fedha za kidigitali unaotumia teknolojia inayoitwa “Blockchain”. Mifumo hii haiendeshwi na benki, na imetengenezwa maalum kutegemeza malipo ya kimataifa bila kuwa na mtu kati. Mpaka sasa kuna Cryptocurrency zaidi ya 2,000 duniani kote mbali na kwamba chache ndizo zimepata umaarufu kama Bitcoin.
- Faida: Kutumia mfumo huu wa malipo kunakupa faida ya kutumia teknolojia mpya na hivyo kupata wateja wenye mwelekeo wa kupenda taknolojia
- Changamoto: Mifumo hii bado haijakubalika na serikali nyingi duniani. Hata hivyo inazidi kuimalika zaidi na kukubalika na wataalam wa fedha wanatabiri kuwa itakuwa na nguvu sana siku za mbele
Peer to Peer
Peer to peer ni mifumo ya malipo ambayo inaruhusu utumaji wa pesa moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kwa kampuni bila kuhusisha mtu kati (third party). Baadhi ya mifumo ambayo imeweka njia hii ya malipo ni CirclePay, Facebook Messenger na Zelle. Mifumo hii haikuanza kwa nia ya kufanyia biashara bali kama njia ya watu kutumiana fedha. Hata hivyo baadhi ya makampuni yanapendelea njia hii kwa sababu ni ya haraka zaidi.
- Faida: Ni njia ya haraka kutuma pesa kwa mtu au kampuni
- Changamoto: Njia hii inaweza kutumika na matapeli hivyo ni muhimu kuwa makini zaidi unapopata mtu au kampuni anayehitaji malipo kwa njia hii.