Jinsi ya kujiunga na One Ecosystem

Je One Ecosystem ni nini?

One Ecosystem ni kampuni ya kimataifa inayotoa elimu ya kidijitali. One ecosystem imesajiriwa nchini Uswisi na ofisi zake zinapatikana  katika mji wa Sofia, Bulgaria.  Biashara ya kampuni hii huzingatia kutoa elimu na maarifa  kupitia mauzo ya moduli za elimu juu ya  mada mbalimbali. Bei za moduli hizi ni kulingana na viwango mbalimbali. Bidhaa hizi  zinauzwa kupitia mtandao wa kimataifa kwa watu duniani kote. Biashara ya kampuni inajulikana kama biashara ya masoko ya mtandao.

Kwa kununua moduli ya elimu, mwanachama (Wakala wa Masoko Binafsi/ IMA) hupokea zawadi kutoka kwa Kampuni kwa njia ya alama (tokens), ambazo humpa haki ya kushiriki katika vikundi vya kuchimba na kubadilisha alama hizo kuwa ONEs (sarafu ya kidijitali). Kila IMA anaweza kutumia ONEs zake kama njia ya malipo ndani ya  One Ecosystem hususani katika  kununua bidhaa na huduma kutoka  katika jukwaa la biashara la One Ecosystem liitwalo Deal Shaker.

Kusajili mwanachama mpya

Uanachama wa One Ecosystem (OES) unapatikana kwa kusajiliwa na mwanachama ambaye tayari ana uanachama wa One Ecosystem. Vile vile unaweza kuwasiliana na ofisi yetu ili kupata msaada wa usajili kupitia barua pepe info@lico.or.tz au kwa WhatsApp +255745737012. Baada ya kukusajili, utatumiwa barua pepe yenye maelekezo ya kuingia kwenye mfumo. Utatumia username na password ulizotumiwa kuingia kwenye mfumo na kuhakikiwa kama maelezo yanayofuata yanavyoelekeza. Fuatana nami katika uzi huu

1. Baada ya kusajiliwa na kupata username na password, au kama wewe ni mwanachama wa OES kwa muda mrefu, fungua adress ya OES au bofya hapa kwenda kwenye adress moja kwa moja. Ukurasa utafungua ukionyesha huduma mbali mbali za OES zikiwemo: 1. One Academy, 2. One Forex, 3. One Charity, 4. One Voyage, 5. One Vita, 6. Deal Shaker. Bonyeza katikati kama inavyoonyesha kwenye picha hapa chini ili kukupeleka kwenye ukurasa wa kuingia kwenye mtandao

2. Baada ya hatua hii itafunguka sehemu ya kuingiza username na password yako kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Ingiza username yako na password kisha bonyeza “Sign in” ili kuingia kwenye mfumo

3. Ukisha login na kufungua account yako, utaona Dashboard inayoonyesha taarifa mbali mbali kuhusu akaunti yako. Taarifa hizi ni kama Profile yako, Muda na tarehe ya siku hiyo, hali ya akaunti yako, kiwango cha ONE ulichonacho, na bonus ambazo umeshapata. Picha chini inaonyesha mwonekano wa akaunti baada ya kuingia.

4. Jinsi ya kuangalia taarifa zako (Profile overview): Kwenye eneo hili utaona taarifa zote kuhusu akaunti yako. Taarifa hizi ni kama

  • Overview: Sehemu hii inaonyesha taarifa za jumla za akaunti yako: Picha yako, hali ya akaunti kama imehakikiwa (verified) au bado, namba ya simu na adress yako
  • Payment details: Sehemu hii inaonyesha taarifa za malipo. Taarifa hizi zinahusu njia ambazo unaweza kupokea malipo kwa kutumia Bitcoin au USDT. Unaweza kufanya marekebisho hapa ili kuweka taarfia za Bitcoin au USDT kama unazo tayari. Kama hauna, iache sehemu hii wazi, unaweza kurudi baadaye. Kuna thread maalum inayotoa maelekezo jinsi ya kulink akaunti yako na Bitcoin na USDT. Unaweza kuifuatilia hapa
  • KYC (Know Your Customer). Huu ni utaratibu unaotumiwa na taasisi za fedha ili kumthibitisha mteja. Utaratibu huu unatumiwa pia na OES ili kuhakikisha kuwa wanachama wote ni watu halali na hawajihusishi na bishara haramu. Katika sehemu hii unaweza ukapandisha (upload) document kama passport kama sehemu ya utambulisho. Baada ya kuupload document zako, zitapitiwa na OES na kuzipitisha (approve) au kuzikataa. Kama taarifa ulizotuma zimekataliwa utahitaji kutuma taarifa nyingine.
  • Password: Sehemu hii inakuwezesha kubadilisha password (nywila) ya akaunti yako kama unahitaji kufanya hivyo. Ili kubadilisha nywila yako bonyeza “Change password”. Mfumo utakutaka kuingiza nywila unayoitumia kwa sasa na nywila mpya. Utaweka zote zinazohitajika na kubonyeza “Change password”
  • Accounts: Sehemu hii inakuwezesha kuona akaunti zote ulizo nazo. Kupitia sehemu hii unaweza kuunganisha akaunti kwa kuhamisha (transfer) ONE kutoka akaunti moja kwenda nyingine. Vile vile unaweza kutengeneza akaunti mpya kwa kubonyeza “Create New Account”.
  • My modules: Hii ni sehemu inayoonyesha wale walioanza kwa kununua mafunzo hapa waliona ni pakeji ipi walilipia. Kama tulivyosema hapo mwanzo OES inatoa moduli za masomo kama sehemu ya kusajili wanachama wapya. Sehemu hii itakuonyesha package gani ulinunua (mfano Starter).
Tags :

Educational

Share This :