Women’s Day Business Expo

LICO Global ilishiriki kwenye maonesho ya bidhaa za wanawake, katika kuendeleza sherehe za siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 mwezi Machi. Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mtangazaji maarufu wa redio ya E-FM, Dina Marios yalifanyika kuanzia tarehe Jumamosi tarehe 9 hadi Jumapili tarehe 10 Mwezi Machi 2024 katika viwanja vya Msasani Beach Club, Dar es Salaam

Maonesho haya yalijumuisha wanawake wafanyabiashara, na wajasiriamali mbalimbali zaidi ya 200, walioonesha na kuuza bidhaa zao kwa wageni zaidi ya 1,000 waliokuja kwenye maonesho. LICO Global kama mdau wa biashara, tulikuwepo ili kuangalia fursa mbalimbali, vile vile kuunganisha biashara kama mkakati wetu unavyosema. Mtangazaji Dina Marious, kupitia mkakati wake wa “Kitchen Party Gala”, alitumia nafasi hii kupromote biashara mbali mbali za wanawake.

Kupitia, jukwaa hili, LICO Global ilipata wasaa wa kukutana na wafanyabiashara, kubadilishana mawazo na mbinu za kibiashara. Vile vile LICO Global, kupitia kampeni yake ya #biashara_kitaa ilipata wasaa wa kuongea na wafanyabiashara mbali mbali kuhusu safari ya biashara yao, matarajio, na kufanya matangazo kupitia page yetu ya biashara_kitaa. Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazoonesha matukio mbali mbali katika event hiyo.

Tags :

Promotion

Share This :

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *