By Neema Ernest
Maonyesho hayo ya biashara yamefanyika katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja Dar es salaam Kuanzia Tarehe 19 hadi 25 Aprili, 2024, ikijumuisha Wafanyabiashara kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Maonyesho hayo ya biashara yamejumuisha biashara na huduma mbalimbali zitolewazo na watu binafsi pamoja na taasisi za kiserikali.
Ikiwa moja ya lengo letu ni kuwaunganisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Kampuni ya LICO GLOBAL ilifanikiwa kufika katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja na kukutana na wafanyabiashara waliokuwa wakiuza Urembo wa asilia, bidhaa za kufuma ikiwemo vikapu, kofia, mikeka na mapochi, nguo za ufundi wa kitamaduni, bidhaa za kutengenezwa kwa udongo, asali mbichi pamoja na korosho.
Maonesho haya kwa ujumla yamefanikisha kukutanisha wajasiriamali kutoka sekta mbalimbali za biashara na muhimu zaidi yameweza kuashiria nguvu ya muungano na ushirikiano wa nchi yetu ya Tanzania hususani katika ngazi ya biashara ambayo ni kiini cha maendeleo ya nchi yetu.